Efm radio na TV-E yaomboleza kifo cha mfanyakazi mwenzao Seth Katende aka bikira wa kisukuma



Efm radio na TV-E yaomboleza kifo cha mfanyakazi mwenzao Seth Katende aka bikira wa kisukuma
Kwa majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote  wa Efm radio na TV-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama Bikira wa Kisukuma kilichotokea Julai 9, 2017  katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Uongozi na wafanyakazi wa Efm radio na TV-E unatoa pole kwa familia ya marehemu na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.

Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwa kuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu Seth Katende mahali pema peponi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 
Amina


Comments