MABINGWA wa England, Chelsea wanamwangalia kwa jicho la tatu kiungo wa Bayern Munich, Kingsley Coman na sasa wanamwinda kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha primier cha msimu ujao.
Matajiri hao wa jiji la Londo wametajwa katika vita ya kumwania kiungo huyo ambaye anawindwa pia na klabu mbalimbali za barani Ulaya.
Daily Star limeripoti pia tarifa za The Blue kuingia vitani kwa ajili ya Coman.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemuelezea kiungo huyo raia wa Ufaransa kama mchezaji anayeweza kupambana katika kikosi cha msimu ujao, hivyo amemweka katika kurunzi la usajili ujao.
Alisema: "Lazima tujipange kwa ajili ya kutetea taji la msimu ujao pamoja na kuhimili mikiki ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya."
"Hivyo mmoja wa wachezaji ninaowaona wana nafasi ndani ya kikosi chetu ni huyo Kingsley Coman, ambaye ni kijana mwenye faida nyingi katika idara ya kiungo, lakini ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati," alisema Conte.
Comments
Post a Comment