Streika wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameonesha ubabeb usiku wa jana kwa kuifungia klabu yake bao moja pale timu hiyo iliposhinda 3-0 dhidi ya Sint-Truiden.
Bao hilo linakuwa bao lake la 20 katika mechi 59 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC.
Kati ya mechi hizo 59, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 41 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 37 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 27 msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, 8 msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.
Comments
Post a Comment