Manchester United iko mbioni kumsajili mchezaji wake wa zamani Michael Keane kutoka Burnley kwa pauni milioni 25.
Imeelezwa kuwa United iko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumnasa sentahafu huyo wa England mwenye umri wa miaka 24 ambaye anawaniwa na vigogo vingine vya Premier League.
Keane ameibuka kuwa mmoja wa mabeki bora katika Premier League tangu alipoondoka United kwa pauni milioni 2 kwenda Burnley Januari 2015.
Wakati inamuuza, United iliweka kipengele cha kulipwa asilimia 25 iwapo Burnley itampiga bei beki huyo kwenda klabu nyingine, hatua inayowapa mwanya kushinda mbio za usajili wa Keane aliyelelewa Old Trafford tangu akiwa na miaka 11.
Comments
Post a Comment