Abdi Banda Awaaga Mashabiki na Wapenzi wa Simba..Adai Ataikumbuka Simba Daima..!!!



Abdi Banda Awaaga Mashabiki na Wapenzi wa Simba..Adai Ataikumbuka Simba Daima..!!!

Beki wa timu ya Simba SC Abdi Banda ameaga rasmi jana baada ya timu yake kushinda Kombe la Shirikisho kwa kuipiga bao 2 kwa moja Mbao FC katika mchezo uliofanyika mjini Dodoma 

Abdi Banda anasema imefika wakati sasa anapaswa kutafuta maisha mengine nje ya klabu hiyo au sehemu nyingine huku akisema atakumbuka mambo mengi mazuri katika klabu hiyo 

"Ahsante Mungu nashukuru kwa hiki ulichotujaalia. Zawadi ya mashabiki wa Simba nawaachia acha na mimi nitafute maisha sehemu nyingine. Nitamiss vitu vingi hasa 'support' yenu na moyo wenu wa uvumilivu ahsanteni sana na kwaherini" aliandika Abdi Banda 


Comments