Wakala wa nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, Eric Olhats amekiri kwamba Manchester United ndio klabu pekee ambayo imeonyesha dhamira kubwa ya kumchukua staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
United inadaiwa kuwa tayari kuvunja rekodi ya uhamisho wa dunia kwa Griezmann kwa kutoa kitita cha Euro100 milioni ambacho kipo katika kipengele cha mauzo katika mkataba wa staa huyo aliyedhamiria kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo, Real Madrid inatarajiwa pia kutoa ofa kwa staa huyo wa zamani wa Real Sociedad ambaye anadaiwa kuwa tayari kuhamia kwa wapinzani wao licha ya kwamba atakuwa na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Atletico.
Comments
Post a Comment