Samatta kaiongoza KRC Genk kupata ushindi Ubelgiji


Samatta kaiongoza KRC Genk kupata ushindi Ubelgiji

Baada ya kuja Bongo na kupiga bao mbili kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Botwasana, Mbwana Samatta amerejea vizuri kwenye klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa kuisaidia kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Lokeren katika mchezo wa play-off wa Kundi B katika ligi ya Ubelgiji.

Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Albert Stuivenberg alifunga goli lake dakika ya 72 likiwa ni goli la pili kwa timu yake. Pozuelo alianza kuifungia Genk goli la kwanza dakika ya 45 huku Boetius akifunga goli la tatu dakika ya 77 na Jose Naranjo akikamilisha goli la nne dakika ya 90.

Genk inaongoza Kundi Blenye timu sita ikiwa na pointi 3 sawa na Kortrijk huku timu zote (6) zikiwa zimecheza mechi moja. Genk inaongoza kundi kwa tofauti ya wastani wa magoli



Comments