ROJO ALIA MUNGU WAKE BAADA YA KUUMIA GOTI NA KUTOLEWA KWA MACHELA


ROJO ALIA MUNGU WAKE BAADA YA KUUMIA GOTI NA KUTOLEWA KWA MACHELA

Manchester United imekumbwa na balaa lingine la majeruhi baada ya sentahafu wake tegemeo Marcos Rojo kuumia na kutolewa nje kwa machela kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht.

Beki huyo wa  Argentina aliumia goti la kushoto dakika ya 20 tu kwenye mechi hiyo iliyochezwa Old Trafford na hakuweza kuendelea.

Picha zilionyesha Rojo alikuwa akiomba dua wakati akitolewa na machela huku nafasi yake ikichukuliwa na Daley Blind.



Comments