PEP GUARDIOLA ALENGA MSHALE KWENYE TIMU YA NICE YA UFARANSA… aonyesha nia kwa kiungo Paul Baysse



PEP GUARDIOLA ALENGA MSHALE KWENYE TIMU YA NICE YA UFARANSA… aonyesha nia kwa kiungo Paul Baysse
BOSI wa Manchester City, Pep Guardiola ameonyesha nia ya kumsainisha kiungo wa timu ya Nice ya Ufaransa, Paul Baysse.

Paul Baysse ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu ndani ya kikosi cha Nice ambayo msimu huu imekuwa katika ushindani mkubwa na timu kongwe za Ligi Kuu nchini humo.

Akinukuliwa, Pep Guardiola amesema anaelekeza kurunzi lake la usajili huku na huko duniani na kwamba Baysse ni kati ya wanandinga anaowaona watakuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Manchester City.

"Ana sifa moja kubwa, nayo ni uwezo wake wa kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani na anajua kujipanga hasa katika mazingira magumu."


"Kizuri ambacho ni sifa ya ziada ni kwamba ni mzuri katika kupanga safu ya ulinzi, hivyo ni mtu muhimu kwa sasa katika kiwango cha soka la dunia," nalizungumza Pep Guardiola na kunukuliwa na The Goal.


Comments