JURGEN KLOPP ATAMANI KUMALIZIA UKOCHA WAKE LIVERPOOL



JURGEN KLOPP ATAMANI KUMALIZIA UKOCHA WAKE LIVERPOOL

Jurgen Klopp amekiri kuwa huenda akamalizia maisha yake ya ukocha Liverpool ingawa anajua kuwa analazimika kushinda mataji kwanza. 

Kocha huyo raia wa Ujerumani amesema hatarajii kufikisha klabu 10 katika kazi yake ya ukocha na hivyo kama atakuwa na mafanikio mazuri Liverpool basi anaweza akaitumikia kwa muda mrefu hadi kustaafu.

 "Kama nitakamilisha mkataba wangu na Liverpool, basi kuna nafasi ya kushinda mataji na huwezi kujua nini kitafuata, " anaeleza Klop.

"Sitakuwa kocha kwa vilabu 10 tofauti kwa maisha yangu yote ya ukocha. Hakuna nafasi finyu kuwa naweza nikafundisha vilabu vitatu tu".

Klop amefundisha FSV Mainz 05 kuanzia mwaka 2001 hadi 2008, Borussia Dortmund mwaka 2008 hadi 2015 ambapo Liverpool inakuwa ni klabu yake ya tatu na pengine ya mwisho.





Comments