Msanii wa filamu nchini Jacob          Stephen maarufu kama JB amefunguka na kusema kuwa kikosi cha          Simba cha hivi sasa si kibaya sana ukilinganisha na vikosi          kadhaa vya Simba ambavyo yeye anavikubali zaidi. 
        JB anadai kuwa katika moja ya          vikosi vya Simba ambavyo vimewahi kumkosha sana ni pamoja na          kile kikosi kilichoipiga Yanga bao 4 
        "Simba ambayo ilinifurahisha          naikumbuka ni ile Simba ya CAF, iliyofika fainali ya CAF Simba          ile niliipenda sana ile ilikuwa ni Simba bora kwangu mimi,          harafu nyuma yake baada ya ile Simba nyingine iliyokuwa nzuri ni          ile ya Captain aliyemaliza muda wake Seleman Matola nayo ilikuwa          Simba nzuri sana ambayo kwa mara ya kwanza iliweza kuwatoa          waarabu kama unakumbuka ni Simba ambayo ilinifurahisha mno"          alisema JB 
        JB alizidi kufafanua vikosi vya          Simba ambavyo kwake vilimkosha kuwa ni pamoja na Simba ile          ambayo Okwi aliingia kwa mara ya kwanza. 
        "Simba ya Okwi wakati anaingia          kwa mara ya kwanza ilikuwa nzuri sana, Simba ile iliyopiga Yanga          goli 4 ilikuwa Simba nzuri, na hata hii Simba tuliyonayo saizi          si Simba mbaya sana lakini zile za nyuma nadhani zilikuwa katika          ubora wake zaidi" JB 
        
Comments
Post a Comment