Bayern Munich wametolewa na Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kulambwa 4-2 katika mchezo wa robo fainali uliokwenda hadi dakika 30 za nyongeza.
Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika Bayern walikuwa wamefanikiwa kulipa kisasi cha bao 2-1 lakini baada ya kwenda 'extra time' Real Madrid wakatupia wavuni mabao matatu.
Mtu aliyefanya kazi kubwa ni Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli matatu. Ikumbukwe pia kuwa Ronaldo ndiye aliyeifungia Real Madrid mabao yote mawili katika mchezo wa kwanza mjini Munich wiki iliyopita.
Robert Lewandowski aliitanguliza Bayern Munich kwa bao la penalti dakika ya 53 lakini Ronaldo akachomoa dakika ya 76 kabla Sergio Ramos hajajifunga dakika mbili baadae.
Ronaldo akafunga dakika ya 105 na 110 wakati Marco Asensio alishindilia goli la nne dakika ya 112. Real Madrid wanatinga nusu fainali kwa kishindo.
Comments
Post a Comment