Ander Herrera amesema ana kiu ya kulipa deni la uaminifu aliopewa na kocha wa Manchester United Jose Mourinho msimu huu.
Kiungo huyo amekuwa mchezaji nguzo kwa United na alikuwa nyota wa mchezo kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea Jumapili iliyopita.
Herrera alimtengenezea pande tamu Marcus Rashford lililozaa goli la kwanza dakika ya saba kabla yeye mwenyewe hajafunga goli la pili ndani ya Old Trafford.
"Nina mshukuru sana Mourinho," anaeleza Herrera. "Msimu huu umekuwa bora na nimekuwa mchezaji wa kudumu kwenye timu yetu.
"Nina furahia maendeleo yangu na nina furaha na kiwango changu."
Herrera alikuwa usajili wa kwanza wa Louis Van Gaal, akitokea Athletic Bilbao mwaka 2014, nyota huyo hakupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha United.
Lakini chini ya Mourinho aliyechukua mikoba ya Van Gaal, Herrera akaibuka kuwa miongoni kwa majina ya kudumu kwenye kikosi kinachoanza.
Kiungo huyo wa Kihispania amebainisha kuwa Mourinho aliongea nae mara tu alipofika Old Trafford na kumuongezea hali ya kujiamini.
"Nina furaha lakini sijamaliza. Hadi sasa kila kitu kinakwenda vizuri kwa upande wangu lakini bado napaswa kuonyeza kile cha ziada ninachoweza kukikfanya," alisema Herrera.
"Nataka kujitoa kadri niwezavyo kwaajili ya kocha na sitazami yaliyopita. Nina furaha sana.
"Alinipa nafasi tangu siku ya kwanza, akanifanya nijiamini na akaniambia nitakuwa nitakuwa mchezaji muhimu katika mipango yake. Nitamshukuru siku zote.
Comments
Post a Comment