Uwanja Wa Shanghai Shenhua Ya Tevez Wateketea Kwa Moto.


Uwanja Wa Shanghai Shenhua Ya Tevez Wateketea Kwa Moto.

Klabu iliyovunja rekodi ya usajili kwa kumfanya Carlos Tevez kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, Shanghai Shenhua ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini China leo imejikuta katika wakati mgumu baada ya sehemu kubwa ya uwanja wake kukumbwa na moto na kuteketea.

Moto mkubwa na moshi ulizigaa ukionekana kuendelea kusambaa katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba jumla ya watu 33,000 asubuhi ya leo Jumanne hivyo kupelekea uwezekano wa klabu hiyo kucheza mchezo wake unaofuata katika viwanja vingine.

Passers-by filmed the fire on their mobile phones as the            black smoke stopped traffic in the streets nearby 

Hata hivyo taarifa zilizotoka zimethibitisha kuwa hakuna mtu aliyeumia katika tukio hilo la moto huku shirika la zima moto likifanikiwa kuuzima moto huo. Mamlaka za mji mdogo wa Hongkou wanachunguza chanzo cha moto huo.

Shanghai Shenhua, inayofundishwa na kocha Gus Poyet, wanaweza kujikuta wakicheza mchezo wao unaofuata dhidi ya Changchun Yatai unaochezwa April 16 katika uwanja mwingine kama marekebisho hayatofanyika kwa wakati.

Shanghai are fourth in the Chinese Super League table,            having won one and drawn one of their games so far

Klabu hiyo ilikamata vichwa vya habari duniani muda mfupi kabla ya mwaka mpya walipomsajili mshambuliaji wa zamani wa West Ham, Manchester United na  Manchester City  kwa gharama inayokadiriwa kufika paundi milioni 71.6.

Akilipwa kiasi cha paundi 615,000 kwa wiki, Tevez ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani katika mkataba wake wa miaka miwili huku hii ikibeba uwezo wa kifedha ambao upo kwenye vilabu hivyo vya China.

 

 

 



Comments