UBABE DHIDI YA MPENZIWE WAMWINGIZA MATATANI LUCAS HERNANDEZ


UBABE DHIDI YA MPENZIWE WAMWINGIZA MATATANI LUCAS HERNANDEZ
BEKI wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez ameamriwa kuitumikia jami kwa muda wa siku 31, baada ya kutiwa hatini kwa kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani.

Adhabu hiyo imekuja kutokana na tukio lililomuhusisha Hernandez na mpenzi wake huyo wa zamani Amelia Llorente Februari 3, mwaka huu.

Habari kutoka nchini Hispania zilieleza jana kwamba mbali na beki huyo pia Llorente nae amepewa adhabu kama hiyo pamoja na faini ya euro 180 kutokana na uharibifu alioufanya dhidi ya gari la Hernandez.

Taarifa hizo zilieleza kuwa mbali na adhabu hizo, wawili hao wameamriwa pia kila mmoja kukaa umbali wa meta 500 kutoka kwa mwenzake na wala wasiwe na mawasiliano ya aina yoyote kwa muda wa miezi sita.


Zilieleza kuwa kabla ya kutolewa adhabu hiyo, awali waendesha mashitaka nchini humo walikuwa wamependekeza kifungo cha miezi saba dhidi ya Hernandez na huku wakitaka Llorente nae aende jela miezi mine.


Comments