KOCHA Sir Alex Ferguson ndiyo nembo iliyoko nyuma ya mafanikio ya Manchester United kuanzia mwaka 1986 hadi 2013 aliwapa karibia kila kombe kuanzia Uingereza Ulaya na Dunia nzima.
Tangu baada ya Ferguson kuondoka timu hiyo imekuwa ikiyumba huku makocha wawili waliomfuata David Moyes na Luis Van Gaal wakishindwa kuwapa kile wanachotaka, huku kocha wao wa sasa Jose Mourinho kidogo akianza kuwafuraisha.
Tayari mashabiki wa Manchester United dunia nzima walianza kupiga kelele wakitaka Ferguson arudi kutetea Jahazi lao linaonekana kuzama kabla ya Morinho kuanza kuwainua.
Lakini sasa kiu ya mashabiki wengi wa Manchester United ya kumuona Ferguson akiwa kwenye benchi la Old Traffold kama kocha inaelekea kutimia, Ferguson atarudi kama kocha wa United Juni 4, mwaka huu.
Ferguson ambaye hadi anastaafu alishawapa United jumla ya makombe 26, atakuwepo kwenye mchezo maalum kwa ajili ya kiungo wa Manchester United, Michael Carrick.
Ferguson katika mchezo huo atakuwa kocha wa wachezaji wa zamani wa Mancherster United.
Ferguson atakuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa zamani wa United ambao watacheza na timu ya Carric.
Pengine hii itawavutia sana washabiki wa Manchester United, kwani toka Ferguson atangaze kuustafu hawajawai tena kumuona akisimama nje ya uwanja kama kocha.
Comments
Post a Comment