CHANZO BIN                          ZUBEIR
            Na Princess Asia, DAR ES SALAAMSIMBA SC                      imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2                      na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom                      Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
             Kwa matokeo hayo,                    Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 55,                    baada ya kucheza mechi 24, wakifuatiwa na mabingwa                    watetezi, Yanga wenye pointi 52 za mechi 23 ambao                    kesho watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja                    wa Jamhuri, Morogoro.
             Mbeya City wao baada                    ya sare leo, wanafikisha pointi 30 baada ya kucheza                    mechi 24. 
             Katika mchezo huo                    uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, hadi                    mapumziko Mbeya City walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0                    lililofungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 37 kwa shuti                    akimalizia kazi nzuri ya Raphael Daudi.                            Shiza Kichuya ameifungia Simba bao la                    kusawazisha kwa penalti dakika ya 86
Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
            Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
 Beki wa kulia,                    Mohammed Hussein 'Tshabalala' alipiga shuti kali                    dakika ya 24, lakini kipa Mmalawi wa MCC, Owen Chaima                    akadaka na Nahodha Jonas Mkude naye alikaribia                    kuifungia Simba dakika ya 28 kama si shuti lake kwenda                    nje baada ya pasi ya winga Shiza Kichuya.
             Mshambuliaji tegemeo                    wa timu hiyo, Mrundi Laudit Mavugo alikaribia kufunga                    dakika ya 32 kama si beki wa Mbeya City, Rajab Zahir                    kuokoa.
             Kiungo Muzamil Yassin                    alipiga shuti zuri baada ya krosi ya Hamadi Juma                    dakika 34, lakini mpira ukapaa juu na dakika ya 40                    mshambuliaji mwingine tegemeo wa Simba, Ibrahim Hajib                    nusura aipatie bao timu yake kama si shuti lake                    kudakwa na Chaima. Zaidi ya bao lao,                    shambulizi lingine la maana Mbeya City walifanya                    dakika ya 25, Ditram Nchimbi akipiga shuti kali baada                    ya pasi ya Bryson Raphael, lakini mpira ukaenda nje.
             Hajib aliisawazishia                    Simba SC kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65,                    uliopigwa nje kidogo ya boksi la Mbeya Ciry baada ya                    Bryson Raphael kuunawa mpira.
             Baada ya bao hilo,                    Mbeya City wakafunguka na kuanza tena kusaka ushindi                    Uwanja wa ugenini na haikuwa ajabu walipofanikiwa                    kupata bao la pili dakika ya 79, mfungaji Nahodha                    wake, Kenny Ally.
             Hata hivyo, Simba SC                    wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya                    aliyefunga kwa penalti dakika ya 86 baada ya Tumba Lui                    kumuangusha beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' kwenye                    boksi.
             Kikosi cha Simba SC                    kilikuwa: Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein                    'Tshabalala', James Kotei, Abdi Banda, Jonas Mkude,                    Ibrahim Hajib/Mwinyi Kazimoto dk80, Muzamil                    Yassin/Mohammed 'Mo' Ibrahim dk54, Laudit Mavugo, Said                    Ndemla na Shiza Kichuya. 
             Mbeya City: Owen                    Chaima, Haruna Shamte, Majaliwa Shaaban, Tumba Lui,                    Rajab Zahir, Sankhani Mkandawile/John kabanda, Raphael                    Daudi, Kenny Ally, Ditram Nchimbi, Mrisho Ngassa/Ayoub                    Semtawa dk69 na Bryson Raphael/Zahor Pazi dk90. 
          
Comments
Post a Comment