RONALDO SI WA KAWAIDA ...UWANJA WA NDEGE WAPEWA JINA LAKE



RONALDO SI WA KAWAIDA ...UWANJA WA NDEGE WAPEWA JINA LAKE

Cristiano Ronaldo amedhihirisha kuwa yuko matawi ya juu baada ya uwanja wa ndege wa Madeira huko Ureno kubadilishwa jina na sasa utajulikana kwa jina lake (Ronaldo).
Kama vile hiyo haitoshi, Ronaldo akatumia fursa hiyo kuwapiga dongo wanaompinga kwa kusema yeye siyo mnafiki.
Supastaa huyo wa Real Madrid alikuwa kwenye kisiwa hicho cha nyumbani kwao ambapo aliichezea Ureno Jumanne usiku kabla ya sherehe ya kuzindua jina jipya la uwanja wa ndege Jumatano asubuhi.
Uwanja huo sasa utajulikana kama 'Aeroporto Cristiano Ronaldo' na tukio hilo lilipokewa kwa hisia tofauti huku Ronaldo akiwaambia wote wanaopinga hatua hiyo kuwa yeye hakuomba jambo hilo.
Georgina Rodriguez kimwana wa Ronaldo naye alikuwepo kwenye sherehe za kuzindua jina jipya la uwanja wa ndege
Sanamu ya Ronaldo ikiwa kwenye uwanja wa  ndege wa Ronaldo (Aeroporto Cristiano Ronaldo) 







Comments