Kilichotokea pale Nou Camp usiku wa Jumatano March 8, 2017 ilikuwa ni historia kwenye mchezo wa marudiano katika michuano ya Champions League ambayo imevunja rekodi ya muda wote iliyokuwa inashikiliwa na Deportivo dhidi ya mabingwa wa zamani wa michuano hiyo AC Milan mwaka 2004.
Mchezo wa kwanza Deportivo ililala kwa bao 4-1 ikiwa ni hatua ya robo fainali lakini wakafanikiwa kuongoza kwa goli 3-0, zikiwa zimesalia dakika 14 huku aggregate ikisoma 5-4, Fran akafunga goli la nne kwa Deportivo usiku huo.
Mechi za raundi ya kwanza ambazo zilimalizika kwa magoli timu kuongoza kwa magoli manne kwenye michuano ya UEFA lakini matokeo yakabageuka kwenye mechi ya marudiano:
- Borussia Monchengladbach v Real Madrid (1985-86 Uefa Cup)
Real waliikaribisha Borussia Monchengladbach kwenye mchezo wa marudiano katika raundi tatu ya Uefa Cup baada ya miamba hiyo ya Ujerumani kushinda 5-1 kwenye mchezo wao wa nyumbani lakini Madrid wakaweza kutengua matokeo kwa kupata ushindi wa magoli 4-0 na kufuzu hatua ya nane bora.
- Leixoes v La Chaux-de-Fonds (1961-61 Cup Winners' Cup)
Leixoes walikuwa wamechapwa 6-2 huko La Chaux-de-Fonds, lakini mabingwa hao wa zamani wa Uswis walishinda 5-0 kwenye uwanja wao wa Estádio do Mar na kusonga mbele kwenye mashindano.
- Partizan v QPR (1984-85 Uefa Cup)
QPR ilishinda 6-2 kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Highbury kwa sababu uwanja wao wa Loftus Road ulikuwa wa nyasi za plastic, lakini wakapoteza game ya pili kwa kipigo cha magoli 4-0 kwenye uwanja wa Belgrade na kutupwa nje ya mashindano kwa sheria ya goli la ugenini.
Comments
Post a Comment