Sergio Ramos amekanusha shutuma zilizotengenezwa kupitia jina lake kwamba alimshutumu Cristiano Ronaldo kwa ubinafsi wake uwanjani.
Gazeti la Hispania Mundo Deportivo lenye maskani yake katika jiji la Barcelona, hivi karibuni liliandika kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid wamechoshwa na ubinafsi wa Ronaldo.
Mundo Deportivo likasema hali ya hewa miongoni mwa wachezaji hao ilichafuka baada ya sare ya 3-3 dhidi ya Las Palmas Jumatano usiku, matokeo ambayo yaliifanya Real Madrid ikabidhi uongozi wa La Liga kwa Barcelona.
Ikadaiwa kuwa Ramos amesema Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyeruhusiwa kutosaidia kukaba pindi mpira unapokuwa kwa wapinzani eti kwa vile tu ana uwezo wa kufunga magoli 60 katika msimu mmoja.
Hata hivyo nahodha huyo wa Madrid amekanusha habari hizo na kusema kila mchezaji kwenye kikosi cha Zinedine Zidane anawajibika vizuri uwanjani.
"Yote hayo ni uzushi mtupu, sijawahi kusema kuwa Ronaldo si mkabaji. Tuna mshikamano wa kutosha."
Comments
Post a Comment