Kadri siku zinavyokwenda ndiyo jinsi                  Manchester United wanavyoonekana bora.Na kadri United                  wanavyozidi kuwa bora ndio Paul Pogba anavyozidi kuwa                  bora.Ubora wa eneo la kiungo cha Manchester United                  umeimarishwa sana na Pogba huku uwepo wa Ander Herrera                  na Michael Carrick vikizidi kumfanya awe bora.                  
              Aina ya uchezaji wa Pogba unawapa United                    faida kubwa sana.Pogba sio aina ya kiungo anayekaa                    sehemu moja kufanya kazi moja,Pogba anakuwa huru sana                    uwanjani akionekana kurudi nyuma kukaba,anavyochukua                    mipira kuipeleka mbele.Lakini Pogba pia anaisaidia                    United katika kishambulia na ndio maana sio jambo la                    ajabu yeye kuwepo kwenye orodha ya wachezaji                    waliogongesha mwamba mara nyingi.
                  Sasa Pogba ameweka rekodi nyingine mpya                    Uingereza.Pogba anakuwa mchezaji wa kwanza katika ligi                    ya Uingereza msimu huu kupiga pasi 1000 katika nusu ya                    eneo la wapinzani.Hii inaonesha jinsi gani kiungo huyu                    alivyo msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya                    Manchester United katika msimu huu wa ligi.Pengine                    hili pia linawafanya United wasijutie kiasi kikubwa                    cha pesa walichotoa kumnunua Paul Pogba.
                  Jambo la kuvutia zaidi kwa Pogba ni                    kwamba anaweka rekodi hii huku wanaomfuata wakiwa                    wamecheza mechi nyingi kuliko yeye.Jumla ya pasi hizi                    alizopiga Pogba ni 1029.Katika orodha hii,viungo 10                    wanaoongoza kupiga pasi hizi yupo mchezaji mwingine wa                    Manchester United Ander Herrera ambaye yuko nafasi ya                    6 akiwa amepiga pasi 827.Hii inaonesha muunganiko wa                    Pogba na Herrera umeleta nguvu mpya Man United katika                    sehemu yao ya kiungo.
                  Wakati Pogba anaongoza kwa pasi nyingi                    kwenye nusu ya wapinzani,anayemfuatia ni Jordan                    Henderson wa Liverpool mwenye pasi 987.Mesut Ozil wa                    Arsenal yuko nafasi ya tatu akipiga pasi 957,David                    Silva wa Man City yuko nafasi ya nne akiwa amepiga                    pasi 930 na Eden Hazard nafasi ya tano akiwa na pasi                    875.
                
Comments
Post a Comment