Mohammed Dewji amepanga          kuiunganisha Simba kwa Juventus ya Italia.
        Tajiri huyo namba moja kwa sasa          hapa nchini alitua Italia katika klabu hiyo mapema wiki hii na          kufanya nao mazungumzo juu ya kuinua soka la Tanzania. Akiongea          na mtandao wa Salehjembe, Dewji amesema, "Wiki hii nilifanya          kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana          wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa          uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo."
        Juventus imekuwa ikishirikiana na          baadhi ya nchi za Afrika katika kuendeleza mchezo huo ikiwemo          Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri.
        
Comments
Post a Comment