Manchester United yaamua Kufungua pochi iwasafirishe Mashabiki.


Manchester United yaamua Kufungua pochi iwasafirishe Mashabiki.

Manchester United ilipangwa na klabu ya Rostov kwenye droo ya hatua ya 16 bora ya Europa League. Na katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kupata sapoti ya mashabiki klabu ya Manchester United imepanga kulipa gharama zote ambazo mashabiki wataingia kulipia Visa za Urusi kwa mashabiki watakaosafiri kwenye mchezo dhidi ya FC Rostov utakaofanyika March 9.

Manchester United watasafiri mpaka Rostov, klabu ambayo ipo umbali wa takaribani maili 2,000 Mashariki mwa Ukraine, kwa ajili ya mchezo wa raundi ya 16 bora na mashabiki takribani 500 wanatarajiwa kusafiri kwa ajili ya mchezo huu.

Klabu hiyo imepanga kulipa kiasi cha paundi 118.20 (£118.20) ambayo ni gharama ya kupatikana kwa Visa ya Urusi ikiwa ni ishara ya kuwathamini mashabiki ikiwa ni kutambua muda mchache wa mashabiki kujiandaa kwani ni wiki tatu tu zilizopo kati ya droo na mchezo wenyewe.

Lakini pia klabu ya Manchester United itatakiwa kucheza dhidi ya Chelsea kwenye robo fainali ya Kombe la FA, ambayo itakuwa machi 13 yaani siku 3 tu baada ya kucheza na Rostov.



Comments