Rekodi ya Manchester United kupoteza nafasi za kufunga magoli inatisha na laiti kama ingezitumia vizuri basi ingekuwa inakabana koo na Chelsea kileleni mwa msimamo wa Premier League.
Katika michezo yake saba ya Ligi Kuu ndani uwanja wake wa nyumbani - Old Trafford na kuishia kwa sare, United imepiga langoni mwa adui mashuti 136.
Katika mashuti hayo 136, mashuti 45 yalienga goli lakini klabu hiyo ikaambulia kufunga mara tano tu.
United imeshindwa kuondoka nafasi ya sita baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Bournemouth, mchezo ulioshuhudia wenyeji wakipoteza penalti iliyopigwa na Zlatan Ibrahimovic.
Kama United ingeshinda michezo hiyo saba ambayo walikuwa na kila sababu ya kufunga, ingejikusanyia pointi 14 za ziada na sasa ingekuwa na jumla ya pointi 63 sawa na Chelsea.
Comments
Post a Comment