Majeruhi yaanza kuitesa Manchester United.


Majeruhi yaanza kuitesa Manchester United.

Hali sii hali ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na majeruhi yanayokiandama kikosi hicho, United wako katika mbio za kutafuta nafasi nne za juu katika ligi kuu ya Uingereza.

Mbio hizo zinaweza kuingia doa kwani hadi sasa wachezaji wa kikosi hicho 7 wanaweza kutokuwepo katika mchezo wao wa ligi mwishoni mwa wiki dhidi ya West Brom.

Hii inaweza kumpa mtihani kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ya juu ya nani aanze katika kikosi cha kwanza. Zlatan Ibrahimovich atakuwa anamaliza adhabu yake ya kadi nyekundu huku Ander Herrera naye akitumikia adhabu.

Phil Jones aliumizwa na Chris Smalling katika mazoezi ya timu ya taifa huku Smalling naye akiumia wakati akiwa na timu ya taifa. Kiungo wa timu hiyo Paul Pogba naye bado anauguza majeraha aliyoyapata kabla hata ya mechi za mataifa kuanza.

Marouane Fellaini naye bado ni majeruhi huku Wayne Rooney naye akiendelea kupona maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yalimfanya atoswe katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Matatizo ya kuumia kwa wachezaji muhimu yanaifanya United kuonekana kama wana kikosi finyu hali inayopelekea matajiri wa United kutaka kuongeza majina makubwa mwishoni mwa msimu.

Tayari United wanasemekana kumalizana mazungumzo ya awali na Antoine Griezman wa Atletico Madrid, lakini pia kukiibuka tetesi mpya kwamba United wanamtaka kwa nguvu zote nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar.

 



Comments