Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wataanza kulipa stahiki ya mshahara wa kila wiki wa beki wa kulia wa klabu ya Everton Seamus Coleman mpaka pale atakapopona majeraha yake ya kuvunjika mguu aliyopata dhidi ya Wales Ijumaa iliyopita.
Coleman alifanyiwa upasuaji jijini Dublin juzi Jumamosi na sasa imeripotiwa kwamba FIFA watakuwa wakilipa mshahara wa Coleman.
Mshahara wa Coleman unatajwa kufikia kiasi cha £50,000 kwa wiki kwa wakati wote ambao atakuwa akiuguza majeraha chini ya sheria ya usimamizi wa Fifa Club Protection Programme.
FIFA Club Protection Programme ni kitu gani? Ni mpango maalum uliozinduliwa May 2012 kusaidia kuwalipa fidia vilabu, kwa kiasi maalum, ikiwa wachezaji wao watapata majeruhi kutokana na matukio yaliyotokea katika mchezo wa timu ya taifa ya wakubwa – mchezo lazima uwe umetambuliwa na FIFA.
Fidia haitohusisha majeruhi ambayo yalipatikana kabla ya mchezo husika au mchezo ambao hautambuliki na FIFA. Mechi za kirafiki na mechi za kujiandaa na mashindano yoyote yaliyo chini ya FIFA – mchezaji akipata majeruhi kwenye mechi hizi basi FIFA hulipa fidia.
Comments
Post a Comment