KOCHA MAURICIO POCHETTINO WA TOTTENHAM ATETA NA RAIS WA BARCELONA …huenda akawa mrithi wa Luis Enrique
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amefanya mazungumzo na rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu wiki hii.
Pochettino na Bartomeu walikutana katika mgahawa mmoja ndani ya jiji la Barcelona, sehemu ambayo kocha huyo wa Spurs anamiliki nyumba aliyokuwa akiitumia tangu enzi zake za kuikochi Espanyol.
Pochettino amekuwa akihusihswa na safari ya kwenda Nou Camp kurithi mikoba ya Luis Enrique ambaye mapema mwezi huu alitangaza kuwa ataachana na Barcelona mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo Spurs, imedai inajua kuhusu mkutano wa Pochettino na Bartomeu na kusema wawili hao ni marafiki wa karibu.
Haikufahamika iwapo Pochettino alipata baraka za Tottenham juu ya kukutana kwake na Bartomeu lakini ni wazi kuwa mkutano huo umezua sintofahamu.
Mwezi Mei mwaka jana, kocha huyo raia wa Argentinian alisaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kukaa White Hart Lane.
Comments
Post a Comment