Hatimaye chama cha soka nchini Ghana, kimeamua kujipanga upya na maendeleo ya soka nchini humo hasa timu ya Taifa ikiwa ni maamuzi baada ya kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo Avram Grant kuamua kuachia ngazi baada ya kufanya vibaya katika timu ya Taifa kwenye michuano ya AFCON.
Maxwell Konadu amechaguliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa timu ya Taifa ya Ghana, akichukua nafasi ya Avram Grant ambaye chama cha soka nchini humo kuamua kutokuongeza naye mkataba baada ya kurudi vichwa chini kule nchini Gabon.
Konadu, alikuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana ambayo ilishinda medali ya shaba kwenye michuano ya Olimpiki ya mwaka 1992 jijini Barcelona, huku akisaidiwa na mtalaamu wa saikolojia Professor J.K Mintah akifanya kazi kama kocha msaidizi wa muda ia. Kocha huyo mwenye miaka 44 alikuwa ndiye msaidizi wa Avram Grant.
Baada ya kikao cha ghafla kilichofanyika kwenye makao makuu ya shirikisho hilo huko Accra, kamati ya watu sita iliundwa ikiongozwa na Rais wa shirikisho hilo Kwesi Nyantakyi iliundwa kwa ajili ya kusaka kocha mpya.
Comments
Post a Comment