Gerrard Pique Atoa Shutuma Nzito Dhidi Ya Real Madrid. Madrid Kumshitaki.



Gerrard Pique Atoa Shutuma Nzito Dhidi Ya Real Madrid. Madrid Kumshitaki.

Kuna jambo kubwa ambalo lilitokea kwenye mchezo kati ya timu ya Taifa ya Hispania dhidi ya Ufaransa kule Paris, nalo ni matumizi yenye mafanikio ya msaada wa Video kwennye maamuzi ya marefarii. Lakini tofauti ba hilo, alikuwa ni Gerrard Pique aliyechafua zaidi hali ya hewa baada ya mchezo huo.

Pamoja na vyombo vingi vya habari kujaribu kuelezea kwa kiasi kikubwa ukaribu wa siku za karibuni kati ya Pique na Ramos, hali imekuwa tofauti baada ya Pique kuchafua mazingira na hali ya hewa ya klabu ya Real Madrid na uongozi wa klabu hiyo ya Bernabeu.

Maoni ya Pique yalishika hatamu baada ya kuwashutumu viongozi wa juu wa Madrid wakiongozwa na Florentino Perez ambaye ni rais wa klabu hiyo. Pique alisema kuwa hapendi mtindo wa maisha ndani ya Madrid kwenye uongozi wao. "Sina shaka na uwezo wa baadhi ya wachezaji wa Madrid na baadhi ni rafiki zangu, lakini pia nisingeweza kufanya kazi Real Madrid," alisema Pique

"Ambacho sikipendi kwa Real Madrid ni namna wale wanaoketi pale juu kwenye box maalumu wanavyoamua mambo mengi kwa nguvu zao kwenye ligi.

" [Lionel] Messi na Neymar walikumbwa na kashfa na kesi nzito zilizokuzwa…lakini Cristiano [Ronaldo] kesi yake ilitupiliwa mbali. Siku zote imekuwa hivyo," Pique alisema baada ya Hispania kushinda 2-0 dhidi ya Ufaransa.

"Sipendi mambo wanayochangia kuamriwa na wanavyochomekea vitu kama klabu, unataka niseme nini zaidi, Pique alionekana kusisitiza kiasi."Karibu wote ni rafiki zangu na hucheza nao karata lakini nafahamu mambo yanavyofanyika."

Pique pia alifunguka kuhusiana na  maneno ya Ramos na Marcelo baada ya Barcelona kurejea na kushinda dhidi ya PSG baada ya wao kudai ilitokana na usaidizi wa waamuzi.

"Kwangu mie siwezi kasirika na maneno waliyosema [Marcelo na Ramos], na naomba wasije kasirika nikisema hilo pia dhidi yao," aliendelea.

Hata hivyo klabu ya Real Madrid imeweka wazi kuwa itakutana kutizama kama kuna uwezekano wa kumfungulia mashitaka Gerrard Pique kutokana na kauli zake dhidi ya uongozi wa klabu hiyo katika kuamua mambo mbalimbali yanayowapendelea wao.

Madrid wamesema haikubaliki kupata shutuma nzito namna hiyo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa Pique alikuwa anamlenga Marta Silva Lapuerta, ambaye ni mwanasheria wa serikali na mkuu wa kitengo cha sheria na mahakama cha Hispania ambaye mara kadhaa amekuwepo kwenye eneo maalumu pale Santiago Bernabeu.

 



Comments