BAYERN Munich wanamtaka Alexis Sanchez kuwasaidia kukabiliana na Real Madrid na Barcelona kwa ajili ya kutawala Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile atakuwa nje ya mkataba mwishoni mwa msimu ujao na mazungumzo juu ya kuendelea kubakia yamesitishwa kwanza.
Mazungumzo yataanza tena mwishoni mwa msimu, lakini Arsenal inaweza kuamua kupata fedha taslim kiasi cha pauni mil 35 ikiwa atakataa kubakia.
Bayern Munich wako mstari wa kwenye foleni kumsaini Sanchez.
Wanasema Carlo Ancelotti yupo kwa ajili ya mkuangalia vipaji vya juu ili kuisaidia klabu hiyo ya Ujerumani kudumisha utawala wao wa ndani.
Pia anataka sura safi juu zitakazokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bayern imekuwa ikitinga nusu fainali za Ulaya kila mwaka katika kipoindi cha miaka mitano, lakini ilishinda ubingwa mara moja tu dhidi ya Borussia Dortmund mwaka 2013.
Kusainiwa kwa Sanchez kunaweza kuisaidia klabu hiyo ya Ujerumani kwa miamba ya Hispania kama Real Madrid na Barcelona kwenye undava wa hali ya juu barani humo.
Nyota wa Real, James Rodriguez ni mbadala kwa Sanchez ikiwa mpango hautaweza kukamilika na Arsenal.
Comments
Post a Comment