Badri Har raia wa Morocco alijipatia umaarufu sana baada ya kuonekana na ukaribu usio wa kawaida na Cristiano Ronaldo.Mambo mengi yalisemwa kuhisu wawili hao lakini picha ambayo Badri alionekana amempakata Ronaldo ilizua mijadala mingi mitandaoni wengine wakimhusisha Ronaldo na ushoga.
Sasa Badri amehukumiwa kwenda jela miqka miwili baada ya kufanya mashambulio kwa watu.Badri mwenye miaka 32 amefanya matukio hayo nchini Uholanzi japokuwa kesi yake ilikuwa ikiendeshwa Morocco.Na sasa kesi hiyo imerudishwa tena mjini Amsterdam ili kujaribu kuharakisha hukumu yake.Na sasa mahakama imemhukumu Badri kwenda kukaa jela miaka miwili.
Mwaka 2012 Badri anatuhumiwa kuhusika katika tukio la kupigana na kumshambulia mtu mjini Amsterdam.Lakini baada ya kufanya tukio hilo Badri tena kwa kutumia chupa alimshambulia mtu katika ukumbi wa starehe unaotajwa kumilikiwa na mtu aitwaye Jimmy Woo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Badri kwenda jela kwani mwaka 2015 alienda jela kwa kosa la namna hii hii.Na kwa kosa hili inaonekana Badri anaweza kukaa jela kwa muda mrefu zaidi.Hii inamaanisha Badri hatamuona kwa kipindi kirefu rafiki yake Cristiano Ronaldo.
Mwaka 2015 jarida la kiarabu liitwalo Aljabar Al Yaum lilisema Cristiano Ronaldo alitenga kiasi cha £ 2400 kwa ajili ya kuchukua chumba cha hotel.Chumba hicho ilisemekana ni katika hotel iitwayo The Pearl Marakech na Ronaldo alitaka kukitumia yeye na Badri.Ripoti zingine zilisema mwaka 2015 Ronaldo alikuwa akitumia ndege yake binafsi aina ya Gulfsteem G200 kusafiri kwenda Morocco kumuona Badri mara 4 kwa mwezi.
Japokuwa kumeendelea kuwa na tetesi zinazomhusisha Ronaldo na ushoga lakinu mpiga soka huyo yeye hajawahi kuongea lolote.Lakini Ronaldo amendelea tu kutoka na walimbwende kwani baada ya kuachana na mrembo Irna Shayk sasa Ronaldo yuko na mlimbwendwe mwingine Georgina Rodriguez.
Comments
Post a Comment