Wachezaji wa Yanga watakaosafiri kwenda Comoro kucheza mechi ya kimataifa


Wachezaji wa Yanga watakaosafiri kwenda Comoro kucheza mechi ya kimataifa

Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho asubui kuelekea nchini Comoro kwenye mji wa Moroni tayari kwa mchezo wake wa kwanza ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Ngaya.

Msafara utakuwa na wachezaji ishirini(20) benchi la ufundi litakua na watu nane (8) pamoja na viongozi wawili (2).

Wachezaji wanaoondoka kesho ni;

Deogratius Munish, Ally Mustafa, Deud Kaseke, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Mwinyi Haji, Saimon Msuva, Geoffrey Mwashuiya, Saidi Makapu, Hassan Ramadhani, Juma Mahadhi, Yusuph Mhilu, Obrey Chirwa, Nadir Haroub, Justine Zulu, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Oscar Joshua na Emmanuel Martin.

Benchi la ufundi wanaoondoka ni:

George Lwandamina, Noel Mwandila, Edward Samwel Bavu, Juma Pondamali, Juma Zakaria Omary, Hafidhi Saleh Suleiman, Mohamed Omary Mwaliga na Jacob Sospeter Onyango.

Viongozi wanaosafiri.

Mussa Mohamed Kisoki (TFf) na Paul Malume (Yanga SC)

Baada ya kikosi kuwasili kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kesho jioni kwenye uwanja utakaochezewa mchezo siku ya Jumapili.

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano.
Young Africans Sports Club
10.02.2017



Comments