Ujumbe wa Bossou kwamba Yanga haijamlipa kwa miezi minne



Ujumbe wa Bossou kwamba Yanga haijamlipa kwa miezi minne

Beki wa kati wa Yanga Vicent Bosou ameandika kwenye ukurasa wake wa Intagram akilalamika kutolipwa mshahara wake wa miezi minne na klabu yake.

Taarifa za ndani ya Yanga zinadai kuwa, Bossou aliondoka kambini wakati kikosi cha Yanga kikijiandaa kuelekea mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Simba kwa madai kwamba hajalipwa pesa zake za mshahara kwa muda mrefu sasa.

"Hakuna tatizo, waambie wanilipe pesa zangu ninachofanya ni kazi yangu. Nimeshafanya kazi kwa miezi minne bila kulipwa chochote halafu bado naambiwa niendelee kufanya kazi," huo ni ujumbe wa Bossou kwa tafsiri ambayo si rasmi.

Jana mtandao huu uliripoti habari ya Bossou kuwa nja panda ndani ya Yanga baada ya kuzozana na viongozi wa klabu hiyo alipogomea mazoezi na kuondoka kambini bila ruhusa maalum.

Bossou hakuwepo hata kwenye benchi la kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Simba Jumamosi dhidi ya Simba, wakati huo Bossou alikuwa amecheza mechi ya mwisho ya Yanga walipocheza mchezo wa kimataifa wa marudiano dhidi ya N'gaya Club ya Comoro.

Sakata la Bossou huenda likapelekea beki huyo wa timu ya taifa ya Togo akaondoka Jangwani kutokana na hali ilivyo sasa kati ya viongozi wa juu na mchezaji huyo.



Comments