Beki wa Zambia 'Chipolopolo', Stoppila Sunzu amesaini mkataba wa miezi mitano wa kuichezea klabu ya Arsenal Tula inayoshiriki Ligi Kuu Russia.
Taarifa zinasema kuwa Sunzu, ambaye ni mchezo wa Lille ya Ufaransa, amesaini mkataba huo na Tula akiwa Uturuki ilipoweka kambi.
Kwa mujibi wa wakala wa mchezaji huyo Nir Karin amesema mkataba huo utamfanya Mzambia huyo kucheza Russia hadi Juni 2017 na baada ya hapo atarejea Lille ambako mkataba wake utamalizika 2019.
Taarifa zinadai kuwa Sunzu alikuwa anatakiwa Ubelgiji, United Arab Emirates, Marekani na Uturiki, lakini klabu hiyo ya Russia ilionyesha kumtaka zaidi.
"Tumechagua Russia na kuziacha Ureno, Uturuki na Marekani kwa sababu hapa kuna ligi yenye ushindani zaidi. Na Juni akimaliza kucheza kwa mkopo atarudi moja kwa moja Lille," anasema Karin.
Sunzu tayari ameshazichezea klabu za Konkola Blades, Zanaco, Chateauroux na TP Mazembe kabla ya kuhamia Sochaux ya Ufaransa na Shanghai Shenhua ya China msimu wa 2015.
Comments
Post a Comment