Siku za Rooney United zinahesabika


Siku za Rooney United zinahesabika

Siku za Wayne Rooney kuwa United inaonekana zinahesabika.Ujio wa Mhiktaryan,Zlatan Ibdahimovich na Athony Martial unaiweka nafasi ya Rooney katika timu hiyo kuwa mashakani.Umri wa Rooney umeenda na kiwango kimeshuka na hii inamfanya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man United.

Rooney ameshawahi sana kuhusishwa kuondoka Man United,haijaanza leo kwa Rooney kuhusishwa na uhamisho wa kuondoka United,kama umfuatiliaji mzuri wa masuala haya utakumbuka msimu wa mwisho wa Alex Ferguson Wayne Rooney alihusishwa na uhamisho wa kwenda Chelsea japo jambo hilo halikutokea.
Lakini sasa tetesi za Rooney kuondoka Man United zimepamba moto sana.Wakati wa dirisha dogo la usajili la January kuliibuka tetesi za Wayne kuhamia ligi ya China.Japokuwa klabu ambayo ilikuwa ikihitaji huduma ya Wayne Rooney haikutajwa kwa kipindi hicho ila ilikuwa ni wazi kwamba Wayne angevutwa China kutokana na nguvh kubwa ya kifedha ya timu za nchi hiyo.
Tianjin Quanjian timu inayonolewa na nahodha wa zamani wa Italia Fabio Cannavaro imekiri kuwahi kufanya na Rooney mazungumzo.Cannavaro amekiri walimuhitaji Rooney japokuwa hafiti katika staili yake ya uchezaji ila walijaribu kutaka kumsajili Wayne Rooney.
Tianjin Quanjian bado wanapewa nafasi kubwa kumnunua Rooney,japokuwa wanasema katika mipango yao ya usajili jina la mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Aubemayang ndio liko juu.Tianjin pia wako na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Nikola Kalinic ili kuweza kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Kocha wa Man United Jose Mourinho amezidi kukuza tetesi za Rooney kuondoka baada ya kukataa kueleza kuhusu usajili wa Rooney.Mourinho aliwaambia waandishi wa habari kama wanataka kujua kuhusu masuala ya Rooney kuondoka United baasi wakamuulize Rooney mwenyewe.Kauli hiyo ya Mourinho imetafsiriwa kama kukosa uhakika kubaki na Rooney msimu ujao.
Dirisha la usajili nchini China linaisha siku ya Jumanne ijayo.Wakala wa Wayne Rooney aitwaje Paul Steford amesafiri hadi China kujaribu kufanya mazungumzo na baadhi ya timu ikiwemo Tianjin.Tayari Wachina wapo tayari kumlipa Rooney £600,000 kwa wiki kiasi ambacho ni mara mbili ya mshahara wa sasa anaopokea.




Comments