Tanzania imefuzu kwa mara ya          kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-17          zitakazofanyika Gabon mwaka huu.
        Serengeti Boys ilifuzu baada ya          kushinda rufaa yake dhidi ya Congo iliyomchezesha mchezaji          aliyezidi umri.
        Tanzania itaingia Kundi B          ikichukua nafasi ya Congo kundi hilo lina timu za Niger,          mabingwa watetezi Mali na Angola.
        Timu nne zinazofanikiwa kuingia          katika nusu fainali zitafuzu moja kwa moja  Kombe la Dunia la          Fifa U17 litalofanyika India baadaye mwaka huu.
        Waziri wa Michezo, Nape Nnauye          aliandika kwenye akaunti yake ya twiter kuipongeza Serengeti          Boys kwa kufikia hatua hiyo.
        "Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenye          fainali za Afrika chini ya umri wa miaka 17. Nia, uwezo na          sababu za kuchukua kombe hili tunazo. Hongera TZ" aliandika          Nape.
        
Comments
Post a Comment