Samatta kacheza dk 90, Genk imepata sare ugenini Europa League



Samatta kacheza dk 90, Genk imepata sare ugenini Europa League

Mbwana Samatta alipata nafasi ya kucheza dakika zote (90) za mchezo wa Uefa Europa League hatua ya 32 bora wakati timu yake Genk ikilazimishwa sare ugenini ya mago 2-2 dhidi ya Astra Giurgiu ya Romania.

KRC Genk walianza kufumania nyavu mapema tu kipindi cha kwanza kupitia kwa Timoty Castagne dakika ya 25 lakini Constantin Budescu akaisawazishiwa Astra dakika ya 43 ikiwa zimesalia dakika mbili kwenda mapumziko.

Genk wakapambanana kupata bao la pili lililofungwa na Leandro Trossard dakika ya 83 laini juhudi zao za kupata ushindi wa ugenini zilizimwa na Takayuki Seto aliyesawazisha dakika ya 90.

Mchezo wa marudiano utakaopigwa majuma mawili yajayo huku Genk ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani ndio utaamua timu gani itasonga mbele kwenye michuano ya Europa League.



Comments