Ronaldo avunja rekodi ya Ryan Giggs.


Ronaldo avunja rekodi ya Ryan Giggs.

Real Madrid walikuwa uwanjani dhidi ya Napoli katika mchezo ulioisha kwa Madrid kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa sifuri.Magoli ya Madrid yaliwekwa kimiani na Toni Kroos,Karim Benzema na mkata wao mkubwa Casemiro huku Ronaldo akitoka uwanjani bila goli.

Pamoja na kuondoka bila goli usiku huo lakini Cristiano Ronaldo usiku huo alivunja rekodi iliyowekwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Ryan Gigs.Ronaldo ndiye aliyetoa pasi iliyoleta goli la Tonu Kroos na assist hiyo kwake ilikuwa ya 31.
Kabla ya mchezo kati ya Real Madrid na Napoli Ryan Giggs alikuwa akishikilia rekodi ya kutoa assist nyingi.Pamoja na kustaafu kucheza soka lakini bado assist zake 30 katika mashindano ya UEFA ilikuwa ngumu kuvunjwa kabla ya mchezaji bora wa dunia kufanya hivyo dhidi ya Napoli.
Ronaldo ambae huu ni msimu wake wa 5 katika mashindano ya UEFA anaweka rekodi yake sasa ya kuwa mchezaji mwenye assist nyingi zaidi katika mashindano ya UEFA.Lakini huenda Ronaldo asifurahie sana rekodu hiyo kwani ana njaa kubwa na goli akicheza dakika 523 bila kuona wavu.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wenye assist nyingi UEFA.
1.Cristiano Ronaldo    31
2.Ryan Giggs                30
3.Lioneil Messi             24
4.Mesut Ozil                  22
5.Zlatan Ibrahimovich  22


Comments