BOSI wa Manchester City, Pep Guardiola ameonyesha nia ya kumsainisha beki wa kati, Lukasz Piszczek.
Lukasz Piszczek ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu, ana kipaji cha kuweza kucheza katika klabu yoyote kubwa, hivyo City haipaswi kumwacha.
"Ana sifa moja kubwa nayo ni kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani na anajua kujipanga hasa katika mazingira magumu."
"Kizuri ambacho ni sifa yake ya ziada ni kwamba ni mzuri katika kupanga safu ya ulinzi, hivyo ni mtu muhimu kwa sasa katika kiwango cha soka la dunia," alizungumza Pep Guardiola na kunukuliwa na The Goal.
"Sikuwahi kumshawishi kwa kiasi kikubwa lakini natambua vyema uwezo alionao ambao ni muhimu kwetu kama klabu kufanya jitihada kumpata na kuimarisha safu ya ulinzi."
"Kama atafanikiwa kutua kwetu nitajisikia furaha kupitiliza kwasababu ndoto ya fikra zangu itakuwa imetimia."
Comments
Post a Comment