OFFICIAL: Ranieri katimuliwa Leicester City



OFFICIAL: Ranieri katimuliwa Leicester City

It was only nine months ago that Claudio Ranieri took Leicester City to the most unlikely title win in English football history. Heck, maybe football history full stop. But now that fairy tale has a fork in it. It's done.

Uongozi wa klabu ya Leicester City umemfuta kazi kocha wao Claudio Ranieri ikiwa ni miezi tisa (9) tangu akiongoze kikosi hicho kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini England maarufu kama EPL.

Leicester imekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya msimu huu ikiwa imefanikiwa kushinda michezo yake mitano tu huku ikiwa haijapata ushindi tangu kuanza kwa mwaka 2017.

Kikosi hicho ambacho kilitikisa msimu uliopita, kipo juu ya mstari wa kushuka daraja kwa tofauti ya pointi moja na timu iliyo nafasi ya 18.

Inaaminika kwamba, maamuzi ya kumfuta kazi Ranieri yalifanyika baada ya kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Sevilla kwenye mchezo wa kwanza ugenini wa hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League.

Siku chache kabla ya kufungwa na Sevilla, Leicester ilitupwa nje ya michuano ya FA Cup na klabu ya Millwall.



Comments