Niko tayari kuondoka Yanga – Manji


Niko tayari kuondoka Yanga – Manji

Manji ameenda mbali sana baada ya jina lake kutajwa miongoni mwa majina 67 ya watu wanaoshukiwa ku-deal na dawa za kulevya, Mwenyekiti huyo wa Yanga amesema yuko tayari kukaa pembeni ya Yanga kama wanachama watapiga kura ya kutokuwa na imani nae.

Manji amesema, kama wanachama wanaona hawana imani nae, waende Jangwani na kuandika majina yao kisha wapige kura ya kutokuwa na imani nae na yeye ataondoka kwenye klabu hiyo aliyoitaja kuwa ni maarufu.

"Wana Yanga kama wanaona mimi sifai, waandike majina yao pale Jangwani  waseme hawana imani na mimi na mimi kesho niko tayari kuondoka Yanga."

"Sina tija ya kuchafua klabu maarufu."



Comments