Mtoto aandika Barua Kumwomba Marehemu Baba Yake, Aongee Na Mungu Mbinguni Liverpool ishinde.


Mtoto aandika Barua Kumwomba Marehemu Baba Yake, Aongee Na Mungu Mbinguni Liverpool ishinde.

Kabla ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Tottenham, Liverpool haikuwa imeata ushindi kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 2017 uanze. Hii ilipelekea kuwapo kwa hisia tofauti na mtoto mmoja wa aliyekua mchezaji wa Rugby wa Afrika Kusini, Joost van der Westhuizen aliamua kuandika barua iliyogusa hisia za wengi akimwomba baba yake "tafadhali mwambie mwenyezi Mungu mbinguni kuwa Liverpool inatakiwa kushinda."

Mchezaji nguli huyo wa zamani wa  timu ya Rugby ya Afrika Kusini maarufu kama Springboks alikutwa na matatizo ya nuroni tangu mwaka 2011 na alikutwa na mauti mapema mwezi huu, tarehe 6 mwezi Februari.

Na mtoto wa Van der Westhuizen anayeitwa Jordan, aliandika barua kwa baba yake, akimwomba aifikishe kwa mwenyezi Mungu kabla Liverpool haijakutana na Tottenham.

Barua ilisambaa kuitia mtandao wa Twitter, baada ya golikipa wa zamani wa Liverpool, Sander Westerveld, kuweka bandiko kwenye ukurasa wake wa mtandao huo akisema "Liverpool imeshinda, hakuna cha ajabu na asante kwa kumwomba baba yako, Jordan!

Kisha akamalizia na "RIP Joost van der Westhuizen".

Kwenye barua hiyo, Jordan anaandika: "Ahsante baba kwa kila kitu lakini kubwa ya yote kuwa bora kwa namna unayoweza!'

"We ni mchezaji bora wa Rugby duniani na mie nataka kuwa mwanamichezo bora kama wewe kwa sababu ulisema natakiwa kupambana na kufanya juhudi."

"Nitakupenda siku zote, iwe mwezini au duniani. Baba tafadhali naomba umwambie Mungu kuwa Liverpool inatakiwa kushinda."

"Nakupenda sana, Jordan xxx"

Van der Westhuizen, ambaye aliichezea Springboks michezo 89, aliagwa kwenye heshima siku ya Ijumaa huko Pretoria.



Comments