LIVERPOOL, TOTTENHAM ZAINGIA VITANI KUUWANIA "MTAMBO WA MABAO" WA LIVER PLATE



LIVERPOOL, TOTTENHAM ZAINGIA VITANI KUUWANIA "MTAMBO WA MABAO" WA LIVER PLATE
LIVERPOOL ya Jurgen Klopp imeingia katika kupigana vikumbo na Tottenham na kujikuta wote wakiwania saini ya mfumania nyavu wa timu ya Liver Plate, Lucas Alario.

Alario yuko katika kiwango cha juu cha soka kiasi cha kuwaingiza vitani klabu hizo vigogo wa Ligi yap rimier.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa ni kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya wakubwa nchini kwao Argentina.

Hatua ya kuitwa kwake kucheza sambamba na Lionel Messi kumempa heshima ya hali ya juu ya kisoka na sasa anawindwa na timu, zikiwemo Liverpool na Spur.

Liverpool wameweka mezani ofa ya pauni mil 12, ingawa klabu ya Liver Plate imebainisha dau la kuuzwa kwa Alario ni pauni mil 15.2.

Kwa mujibu wa jarida la The Sun, azma  ya kocha Jurgen Klopp amevutiwa na straika huyo lakini hata hivyo ameweka mezani ofa ya pauni mil 8.5, fedha ambayo Liver Plate wanaikataa.


Pamoja na Liverpool na Spur pia timu za Inter Milan na Torino za nchini Italia zimo katika mawindo ya saini ya Alario.


Comments