Mara baada ya Yanga kuchezea kipigo            cha mabao 2- kutoka kwa mahasimu wao Simb, Kocha Msaidizi wa            Yanga Juma Mwambusi amefunguka sababu za timu yake kupoteza            mchezo mojawapo ikiwa ni kuumia kwa kiungo wake Thaban            Kamusoko.
        Mwambusi            amesema kuumia kwa Kamusoko kuliwafanya Simba waje zaidi            katika eneo la katikati, jambo ambalo liliwasaidia kupitisha            mipira kirahisi na hatimaye kuweza kupata mabao mawili na            kuibuka na ushindi.
        Amesema            licha ya kumuigiza Said Makapu kuchukua nafasi ya Kamusoko,            lakini hakufanya kazi ipasavyo, na pia anapungukiwa baadhi ya            vitu alivyonavyo Kamusoko ikiwa ni pamoja na kuwa na maono            pamoja na kuunganisha safu ya nyuma na mbele.
        Sababu            nyingine aliyoitaja Mwambusi ni umakini wa wachezaji wote            kwenye timu yake kupungua na kushindwa kukaba, jambo            lililofanya wawe wanakaba kwa macho.
        "Wao Simba waliongeza namba                katikati, sasa na sisi vijana wetu tuliowaingiza baada ya                kamusoko kuumia walipaswa walitakiwa kuongeza namba                katikati lakini wakashindwa,.... Pia umakini wa ukabaji                kwa wachezaji wetu haukuwa mzuri, Simba walikuwa wanakuja                wanapita watu wanawasindikiza kwa macho" - Amesema Juma                Mwambusi.
        Hata hivyo            amesema matokeo hayo inagawa yanawaumiza, hayajawapotezea            lengo lao la kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania na kwamba            atakaa na walimu wenzake kurekebisha makosa ambayo            yamejitokeza ili yasijirudie tena.
        Katika            mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mavugo na Kichuya            kipindi cha pili, huku la Yanga likifungwa na Msuva kwa njia            ya penati, katika dakika ya 5
        
Comments
Post a Comment