Kocha African Lyon amekubali kucheza na Simba ‘kwa shingo upande’



Kocha African Lyon amekuli kucheza na Simba 'kwa shingo upande'

Kocha wa kikosi cha Africans Lyon Charles Otieno amesema wapo tayari kupambana hiyo kesho japo taarifa za uwepo wa mchezo huo alichelewa kuzipata kutoka wa viongozi wake.

"Wachezaji wapo kwenye hali nzuri ila juzi tulipata majeruhi wachache lakini tutaangalia daktari atasema nini maana kama unavyojua mechi dhidi ya Simba hatukuwa nayo kwenye ratiba yetu ila tumepata taarifa Jumatatu usiku kuwa Alhamisi tutacheza lakini sisi tulikuwa tunaangalia mechi yetu na Ndanda siku ya Jumapili huko Mtwara," – Charles Otieno.

"Tumezungumza na uongozi kuwa mechi hii tumekurupushwa lakini kuna barua walipata hakuna mabadiliko na sisi kwa sababu hii ndiyo kazi yetu, tutaendelea kufanya kazi ili kuona tutatoa matokeo gani kwenye mechi hiyo dhidi ya Simba."

"Ni muda mfupi sana ukizingatia tumecheza Jumapili juzi tulipumzika kwa hiyo jana tulianza mazoezi na leo hivyo tuna siku mbili za kujitayarisha kwa ajili ya mechi hiyo."

"Lakini imetuyumbisha kwa sababu akili nyingi tulikuwa tumeweka kwenye mchezo dhidi ya Ndanda lakini mpaka sasa hivi hatujui kama mechi yetu na Ndanda imesogezwa mbele au vipi, sisi tutacheza na Simba ili tuone nini kitatokea baada ya dakika 90."



Comments