Kiduku chamtia matatani Asamoah Gyan uarabuni.


Kiduku chamtia matatani Asamoah Gyan uarabuni.

Asamoah Gyan mchezaji wa timu ya taifa ya Ghana ambae kwa sasa anakipiga Dubai katika timu ya Al Ahli ambapo yupo kwa mkopo akitokea Shanghai SIPG ya China ni kati ya wachezaji mabishoo sana.Gyan kama kijana nje ya soka huwa anapendelea sana mambo ya mitindo na muziki na hata muonekano wake huwa uko kisanii sanii.

Sasa ubishoo wa Gyan unaelekea kumtokea puani huko Uarabuni.Waarabu wana sheria zao sana katika nchi zao na moja ya sheria zao ni kuhusu unyoaji wa nywele.Gyan amekutwa na hatia katika unyoaji wake wa nywele na sasa itamlazimu kukaa nje ya uwanja hadi hadi hapo atakapobadili staili yake ya nywele.
Sio Gyan tu aliyekutwa na kadhia hiyo kwani kuna wachezaji wengine 40 ambao nao wamekumbwa na suala kama hili.Sheria za waarabu nchini humo zinakataza unyoaji wa style ya kunyoa pembeni ya kichwa na kuacha tu nywele juu ya kichwa almaarufu kama kiduku,mtindo ambao Gyan amekuwa akiutumia sana.
Mwaka 2012 golikipa wa timu moja huko Duba aitwaye Waleed Abdullah alitolewa nje kabla ya mechi kuanza akitakiwa akanyoe vizuri nywele zake.Gyan alionekana katika mashindano ya kombe la mataifa Afrika akiwa kanyoa kiduku chake huku pembeni akiwa amechonga herufi ya W.Hii ni kama majanga yanaendelea kwa Gyan baada ya kushuhudia timu yake ya taifa ikiondolewa katika mashindano ya mataifa Afrika kwa kipigo cha bao mbili toka Cameroon.


Comments