Kesi Za Kodi Kuwazuia Messi na Neymar kucheza UEFA, Nchini Uingereza


Kesi Za Kodi Kuwazuia Messi na Neymar kucheza UEFA, Nchini Uingereza

Nyota wa Barcelona Lionel Messi na Neymar wanaweza kunyimwa nafasi ya kuingia Uingereza iwapo watafuzu kuingia kwenye hatua inayofuata na kufuzu fainali kutokana na kesi zinazoendelea za makosa ya ukwepaji kodi.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema kuwa anahofia wachezaji hao wanaweza wasiweze kuingia Cardiff ambapo mchezo wa fainali wa UEFA mwaka huu utafanyika kwenye uwanja wa  Principality Stadium mwezi Juni iwapo tu watafanikiwa kufuzu.

Hata hivyo itakuwa kama maajabu Barcelona kuingia kwenye fainali ya mwaka huu ya mwezi Juni kwani tayari wameshafungwa mabao  4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 dhidi ya Paris Saint-Germain.

Mapema msimu huu, beki wa PSG, Serge Aurier alinyimwa ruhusa ya kuingia Uingereza kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates mwezi Novemba kutokana na kuwepo kwenye rufani ya kesi ya kudhuru.

Lakini pia hali ya kisiasa inayohusu mpango wa Brexit ikiendelea kuwepo, Ceferin anaamini kuwa England itakumbana na tatizo kubwa kwenye mpango wa kutaka kuandaa mashindano ya Mataifa ya Ulaya mwaka  2028 au kombe la Dunia mwaka 2030.



Comments