JUVENTUS YAMMALIZA NGUVU JURGEN KLOPP KWA WINGA WA LEVERKUSEN



JUVENTUS YAMMALIZA NGUVU JURGEN KLOPP KWA WINGA WA LEVERKUSEN
INGAWAJE hakuwahi kabisa kusaini katika kikosi cha Liverpool, lakini winga Julian Brandt alikuwa anatarajiwa kwamba anakwenda kukipiga katika kikosi hicho.

Rafiki zake wote na ndugu zake walikuwa wanajua kwamba winga huyo wa Bayer Leverkusen alikuwa amekamilisha mambo muhimu kujiunga na Liverpool.

Hata hivyo habari mbaya kwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye ndie alikuwa anakamilisha mambo muhimu kwa Julian ni kwamba nyota huyo anakwenda Juventus ya Italia.

Haya ni kama maumivu makali kwa Klopp na sasa anatakiwa kufanya kazi ya ziada kubadilisha tena mawazo na msimamo wa nyota huyo wa Ujerumani.


Inadaiwa kwamba Klopp alichokuwa anakisubiri ni kumtambulisha tu winga huyo na habari hizi mpya zinaweza kumfanya akose usingizi kwa muda mrefu.  


Comments