JAMIE CARRAGHER AMMIMINIA SIFA HENRIKH MKHITARYAN... awapond Ozil, Silva, Mata



JAMIE CARRAGHER AMMIMINIA SIFA HENRIKH MKHITARYAN... awapond Ozil, Silva, Mata
MCHAMBUZI wa michezo katika runinga ambaye ni nyota wa zamani wa klabu ya Liverpool, Jamie Carragher amesema uwezo wa mchezaji Henrikh Mkhitaryan uko juu kwa sasa.

Mkongwe huyo amesema kwamba uwezo wa kiungo huyo umewafunika kabisa nyota wengine wanaotakata katika Ligi Kuu ya Uingereza wakiwamo Ozil, Silva na Mata.

Akizungumzia kuhusu uwezo wa nyota huyo wa Manchester United ambao ameuonyesha kwenye mechi dhidi ya Leicester City, Jamie alisema Mkhitaryan ana kitu ambacho ni wachezaji wachache sana walionacho.

Kwa mujibu wa nyota huyo, kitu chenyewe ni uwezo wa kuwa na kasi inayofanana na kwa muda wote.

Amesema wachezaji kama Mesut Mustafa Ozil wa Arsenal, Juan Manuer Mata Garcia wa Man United, David Josue Jimenez Silva wa Man City, ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana kwenye kutoa pasi lakini Mkhitaryan yupo kwenye kiwango kingine kabisa.


Mkhitaryan amekuwa chaguo kubwa kwenye kikosi chake na uwezo wake mkubwa umekuwa ukiwafurahisha washabiki wengi kutokana na kasi na aina ya pasi anazotoa.


Comments