Wakati Jose Mourinho anaanza kazi ya ukocha na klabu ya Manchester United kuliibuka maswali mengi kuhusiana na namna alivyokuwa anaendesha klabu. Ilikuwa wakati mgumu hasa wengi wakirejesha kumbukumbu za matokeo yake akiwa na klabu ya Chelsea na namna alivyoondolewa klabuni hapo.
Sir Alex Ferguson aliwahi kuwaeleza wafanyakazi wenzie kuwa alifikiri siku zote kuwa Mourinho alikuwa kocha ambaye klabu yenye chapa kama ya Manchester United walikuwa wanahitaji kuwa naye. Aliwahi kunukuliwa akisema "tulimhitaji kipindi kirefu miaka kadhaa iliyopita."
Kinachovutia kwa sasa kwa Mourinho ni mbinu alizochukua katika kuimarisha klabu hiyo. Ferguson anakiri kufurahishwa na namna ambayo Mourinho kajitahidi kubadili viwango vya wachezaji mmoja mmoja kuanzia kwenye viwanja vya mazoezi na uchaguzi wa timu. Lakini pia Mourinho kabadili mengi pale Carrington ambayo hayakufanyika mwanzo.
'Kuanzia kwa mapokezi mpaka kwa wapishi, wengi ni walewale,' lakini kiutendaji wapo tofauti.
Tofauti yake na kipindi akiwepo Louis van Gaal ni hali ya hewa na mwenendo mzima kiuongozi ilivyobadilika kwa Manchester United.
Chanzo cha ndani kinasema kuwa kwenye eneo la chakula kuna skrini maalumu ambayo hutoka na inaweza kukufanya kuchanganua na kutenganisha kwa urahisi kati ya wachezaji na watu wengine. Hii inarudisha nyuma kumbukumbu za Ferguson, ni tofauti na ilivyokuwa wakati wa Van Gaal.
'Louis angeweza kutumia kitu hiki wakati akielekeza kitu kwa wachezaji au kukiwa na kikao cha wachezaji kuelekea kwenye mchezo wa uwanja wa ugenini. Jose Mourinho hafanyi hivyo, kila mmoja anakula na mwenzie.'
Wachezaji wanakubali na wanayafurahia mazoezi chini ya Mourinho. Mazoezi yanahusu matumizi ya mpira tofauti na ilivyokuwa kwenye uongozi wa makocha waliopita, na Mourinho amekuwa akiongeza uhai kwenye mazoezi kwa kuhakikisha kuwa kuna mashindano tofauti na kuwashindanisha mastaa jambo ambalo linawaongezea ushindani dhidi ya kila mmoja.
Wachezaji hujigawa kwenye makundi na kuwa tayari kwa mashindano tofauti. Mfano Rooney anaweza kuongoza kundi lake wakifanya mazoezi kuushinda muda waliowekewa ili wawe washindi.
Hii haina maana kuwa mazoezi yameshuka kiwango, ni tofauti na hilo. Mourinho, kama ilivyokuwa kwa Pep Guardiola, anazingatia mazoezi na anahakikisha anaingiza hali ya kukubaliana na kupendana.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya St. Etienne kwenye Europa League, Mourinho alimualika Eric Bailly, kuzungumza na waandishi baada ya yeye kuzungumza na Mourinho hakuondoka tu, bali alichukua picha za Bailly na kuwatumia wachezaji wenzie.
Kabadilika, hata utani dhidi yake umekuwa ukimchekesha tofauti na wengi walivyomdhania mwanzo, kuna wadadawa sehemu ya kulia chakula ambao mwanzo walihofia kumsemesha wakimwona mtu ambaye alikuwa kama amebeba dunia mabegani mwake.
Baada ya klabu kutangaza kuwa wanaanzisha uhusiano na kampuni inayoongoza kwa kuzalisha saa, wachezaji walishangazwa na Mourinho kutokea wakati wala hakutegemewa kufika. Hivyo ndivyo Mourinho alivyobadilika kwa namna anayojihusisha na wachezaji.
Comments
Post a Comment